IDARA ya uhamiaji nchini imewataka watanzania kupuuza habari zinazozagaa kuhusu uvumi wa pasipoti mpya kuwa zimechakachuliwa.
Kauli hiyo imetolewa jana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dkt. Anna Makakala jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema wananchi wanatakiwa kupata taarifa sahihi kila mara juu ya kila jambo linalohusu maendeleo yao na mambo yanayoletea ustawi wa Taifa , na kwamba wao Idara ya Uhamiaji ndio wenye taarifa sahihi zinazohusu Mchakato mzima wa Pasipoti Mpya za Kielektroniki
Alisema wananchi wanatakiwa kupata taarifa sahihi kila mara juu ya kila jambo linalohusu maendeleo yao na mambo yanayoletea ustawi wa Taifa , na kwamba wao Idara ya Uhamiaji ndio wenye taarifa sahihi zinazohusu Mchakato mzima wa Pasipoti Mpya za Kielektroniki
Hivi
karibuni Rais Dkt. John Magufuli wakati akizindua hati mpya za
kusafiria alisema kumekuwapo na wahujumu wa mchakato huo ambao
hawakufanikiwa kuiba sh. bilioni 400.
Alisema
kumekuwapo na watu waliozunguka kila kona na kutumia kila njama zote
kupiga vita mchakato huo wakidhani watafanikiwa kuhujumu serikali.
Dkt.
Anna Makakala alisema hatua hizo za kutoa na kueneza taarifa zisizo
sahihi zinawaletea mkanganyiko wananchi na kudhoofisha mawazo na fikra
chanya kwa Taifa lao
Alisema
ni vyema jamii ikatambua kuwa mchakato wa Pasipoti mpya ya kidigitali
ni hatua kubwa kwa Taifa hili na si vyema kuutolea Taarifa zisizo
sahihi. Aliwasihi wanahabari kupata taarifa kutoka katika vyanzo sahihi
na kuzifikisha kwa walaji ambao ni Wananchi.
Alisisitiza
hatua ya mafanikio ya matumizi ya hati hizo hazitarudi nyuma kwa sababu
ya kuwapo na taarifa zisizo sahihi zenye lengo la kupotosha ukweli wa
mchakato huo.
“Ni
vyema jamii kuelewa kazi ya hati hizo ni kulinda usalama wa nchi yetu,
hivyo Uhamiaji tutaendelea kudhibiti mipaka ya Tanzania na kulinda
usalama wa nchi kwa kuwezesha jamii na raia wa kigeni kufuata taratibu
katika utokaji,ukaaji na uingiaji wa kila mmoja,” alisema Dkt. Makakala.
Alisema
kila nchi yenye kuhitaji maendeleo ni muhimu kutumia hati ya kusafiria
ya kielektroniki ili kufikia mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
“Mabadiliko
ya kidunia katika maendeleo yanatuonyesha wazi kuwa Taifa hili
limefikia kuwa na hati za kisayansi na kiteknolojia hivyo katika hati
mpya,mtu yeyote hataweza kutumia ujanja au kughushi na kutumika kwa
matumizi yasiyo sahihi,” alisema Dkt. Makakala.
Alisema
anaamini idara hiyo haitashindwa na wachache wanaokubali kutumika
kuhujumu mchakato huo kwa maslahi binafsi kwakuwa kushindwa kwa mchakato
huo ni kupunguza hadhi ya usalama wa nchi.
“Pasipoti
ndio kitu kinachotuwezesha kudhibiti wanaoingia nchini na kutoka, hiki
ni kitambulisho cha raia sehemu yoyote duniani wenye Pasipoti za
Tanzania ni mabalozi wa Tanzania.
" Mfumo huu utawezesha kudhibiti ujanja wote unaotumika, kutakuwa na cheap na security features nyingi. Sifa ya Taifa letu dunia imeharibika lazima kufanya maamuzi kwa maslahi ya Taifa letu,” alisema.
" Mfumo huu utawezesha kudhibiti ujanja wote unaotumika, kutakuwa na cheap na security features nyingi. Sifa ya Taifa letu dunia imeharibika lazima kufanya maamuzi kwa maslahi ya Taifa letu,” alisema.
Dk.
Anna alisema kufanikiwa kwa mradi huo wa e-Immigration kwa gharama ya
dola za Marekani milioni 57 imekuwa mwiba kwa vigogo walioondolewa
Uhamiaji na sasa wanahaha kwa aibu wakidai kwamba gharama iliyotajwa ni
kwa ajili ya mradi mmoja tu wa e-Pasipoti.
“Ni
wajibu wa kila mtanzania kuwa macho na wale wote wanaotumiwa na
mafisadi kwa ajili ya kuichafua serikali kwakuwa imezuia na kupambana na
uhujumu uliotaka kujitokeza,” alisema.
Alisema
hati hizo zitawezesha waliopotelewa na hati zao kutumia mfumo wa
kiteknolojia na kupakua app yake hata katika simu ya mkononi, hivyo
kutambulika na kupewa msaada haraka kokote duniani.
Alisema hati hiyo inaviwango vyote vya ubora wa kimataifa pia itatumika kama kitambulisho kwa nchi za Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment