Mbunge
wa Temeke kwa tiketi ya (CUF) Mhe. Abdalah Mtolea ameibua sakata la
kusamehewa Babu Seya na mwanae, Johnson Nguza 'Papii Kocha' na kusema
halikuwa jambo jema kwa kuwa watu hao mahakama iliwabaini kuwa ni
wabakaji.
Mtolea
amesema hayo jana Februari 7, 2018 akiwa bungeni na kudai kitendo cha
watu hao kuachiwa na kupewa heshima na Serikali ikiwa pamoja na
kuwapandisha kwenye majukwaa mbalimbali na kuwapa ufadhili haileti picha
nzuri kwa jamii.
"Kwenye
maadhimisho ya Uhuru wa Tanganyika ukatoka msamaha kwa Babu Seya na
wenzake watu ambao pasipo na shaka mahakama zilithibitisha kwamba hawa
watu ni wabakaji sasa tunapokuwa tunasamehe wabakaji uko wapi ulinzi wa
watoto wa taifa hili,tunawapandisha kwenye majukwaa wafanye show yaani
tunawaona kwamba ni kioo cha jamii je wanafundisha nini? Alihoji
Mhe.
Mtolea aliendelea kusema kuwa "Je, mnataka kwamba siku ya mwisho
tukiwauliza watoto ukiwa mkubwa unataka kuwa kama nani aseme nataka kuwa
mbakaji?
Babu
Seya na mwanaye Papii wanategemea kuachia kazi yao mpya muda si mrefu
baada ya kuiaanda mara tu baada ya kupewa msamaha na Rais John Pombe
Magufuli
0 comments:
Post a Comment