Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Kamanda
wa polisi mkoani Pwani (ACP) Jonathan Shanna ,ametoa onyo kwa watu
wenye tabia ya kufunga barabara kwa kuchoma matairi katika mkesha wa
mwaka mpya na kupelekea usumbufu kwa watuamiaji wengine wa barabara
kuacha kufanya kitendo hicho .
Amesema
atakaejaribu kuchoma moto matairi kwenye mkesha huo,jeshi la polisi
mkoani hapo litamchukulia hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine.
Akizungumza
na waandishi wa habari kuhusiana na hali ya kiusalama inavyoendelea
hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye sikukuu ya mwisho wa mwaka
,kamanda Shanna alisema wanazidi kuimarisha doria katika pande zote za
mkoa huo.
Alisema
kipindi cha sikukuu ya x-mas hali ilikuwa shwarii hivyo wanaendelea na
misako ya miguu kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama
na doria hizo zitakuwa mtaa kwa mtaa na nyumba kwa nyumba ili
kuhakikisha watu waishi kwa amani .
Akielezea
kuhusiana na hali ya uhalifu katika kipindi cha Januari hadi disemba
mwaka huu ndani ya mkoa huo ,kamanda Shanna alisema wamefanikiwa
kupunguza idadi ya makosa kwa kiwango kikubwa.
Kamanda
huyo alisema,matukio ya makosa ya uvunjaji yamepungua kutoka 771
kipindi kama hicho 2016 na kufikia 233 mwaka huu ikiwa ni tofauti ya
matukio 538.
Makosa
mengine ni yale ya unyang’anyi wa kutumia silaha ambayo yamepungua
kutoka 31 mwaka jana hadi nane kwa mwaka 2017 tofauti makosa 23.
“Unyang’anyi
wa kutumia nguvu yameripotiwa makosa 43 ,kipindi kilichopita ilikuwa
112 tofauti makosa 69,:;na mauaji makosa yaliyoripotiwa januari hadi
disemba mwaka huu ni 34 ,mwaka uliopita ilikuwa 126 tofauti ni makosa
92.” alifafanua kamanda Shanna.
Aliwataka
wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo mara wanapotilia shaka kundi
ama mtu ni mhalifu ,kwani kila mmoja ana wajibu wa kudhibiti vitendo vya
uhalifu .
Kamanda Shanna ,alisema Pwani yenye utulivu,amani ,yenye kushikamana inawezekana endapo kila mmoja atatimiza wajibu wake.
0 comments:
Post a Comment