Na Bonfasi Mwafulilwa.
wananchi wa kijiji cha Ihanga kata ya Ukwama
wilayani makete mkoani njombe wamelaani vikali kitendo cha kamati ya kijiji
hicho kutumia fedha za ujenzi wa choo cha wanafunzi katika shule ya msingi
Ihanga kutumia katika miradi mingine hali iliyopelekea kusimama kwa ujenzi wa
choo hicho.
hayo
yamejitokeza hii leo february 7,2018 katika kikao cha serikali ya
kijiji cha Ihanga wilayani Makete Mkoani Njombe kilicholenga kujadili
mambo
mbali mbali likiwemo suala la sababu zilizopelekea kusimama kwa ujenzi
wa choo
cha wanafunzi katika shule ya msingi Ihanga.
miche ya parachichi za kupanda shuleni hapo.
kufuatia
maelezo hayo wananchi wa kijiji cha Ihanga kata ya Ukwama
hawakupendezwa na maelezo hayo kwa kwa kuwa mipango ya pesa hizo ilikuwa
kujengea choo cha wanafunzi shuleni.
Kutokana na kujitokeza kwa hali ya wananchi
kutokuwa na imani na suala hilo mh, diwani wa kata hiyo Agustino Tweve
akamwagiza mwenyekiti wa kamati ya shule kukaa na kamati yake ili waweze
kulifuatilia suala hilo huku akitoa siku saba za kufanya uchunguzi huo.
kwaupande wake mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Philipo Sanga amegoma kufanya jambo hilo huku akidai hatua zozote
zitakazochukuliwa dhidi yake yuko tayari kuupokea.
Mheshimia diwani Tweve baada ya kusikia kuwa
mwenyekiti wa kamamti ya shule bwana Philipo Sanga kukaidi agizo lake amesema
sheria kali itachukuliwa endapo ataona utekelezaji wa sula hilo ambalo
linalalamikiwa na wananchi halitafanikiwa.
0 comments:
Post a Comment