Home » » TANGA RAHA- Sehemu ya Kwanza (1)

TANGA RAHA- Sehemu ya Kwanza (1)

Unknown | Sunday, February 11, 2018 | 0 comments
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
Ni siku ya utambulisho mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari moja jijini Tanga nikiwa mimi na mwalimu mwenzangu ambaye wa kike ambaye ndio tumetoka chuo cha ualimu na kupangiwa shuleni hapa
Akaanza mwenzangu kujitambulisha ambaye, akapigiwa makofi na wanafunzi kisha nikafwatia mimi kujitambulisha

"Mimi ninaaitwa Sir Eddy nitafundisha Biology na Chemisty"
Wanafunzi wote wakapiga makofi ma vigelegele hukt wakionekana kupendezwa na utambulisho wangu mfupi na wakueleweka.Muda wa masomo nikakabithiwa kuanza na kidato cha nne katika somo la Biology ambao ndio nao wanaanza mwezi wa kwanza wa muhula wa masomo.Nikaanza kuuliza mwanafunzi mmoja mmoja jina lake ili kuniwia rahisi kuwafundisha na kuwazoea kwa haraka
Nikaanza kipindi huku nikiwauliza uliza maswali ya mada walizo zisoma wakiwa kidato cha tabu, ili niweze kwenda nao sawia kwenye kufundishana
"Ulisema unaitwa nani, binti?"
"Rahma"
"Ehee elezea Reproduction(uzalishaji) kwa mwanadamu inakuwa vipi?"
Akanza kuelezea hatua moja baada ya nyingine kuanzia mtoto anavyo tafutwa hadi kuzaliwa bila hata kukosea.Wanafunzi wenzake wakampigia makofi huku wengine wakitaka kutokana na baadhi ya vitu alivyokuwa akivizungumza
Wakanipa ushirikiano mzuri hadi nikamaliza kipindi na kurudi zangu, ofisini nikisubiri kwenda darasa jengine
Muda wa kutoka ukawadia nikabeba begi langu lenye laptop yangu niliyo hifadhi vitu vyangu mbalimbali
"Sir ninaweza kukusaidia kubeba begi?"
"Rahma ndio unaweza kunisaidia"
Rahma yupo na mwenzake ambaye sikumuona darasani wakati nilipokuwa ninafundisha somo langu
"Unakalia wapi?"
"Maeneo sijui wanapaita Chuda, kitu kama hicho"
"Sir Eddy kwani Tanga wewe ni mgeni?"
"Nimgeni nina kama siku ya nne leo, tangu nije bado majina yana nisumbua sumbua kuyashika"

"Umetokea wapi?"
"Arusha"
Tukatembea njia nzima huku tukizungumza mambo mengi, kuhusiana na mji huu ambao nyumba zake zimepangika vizuri kwa mpangilio wa mistari mistari, nitofauti sana na mji kama Dar es Salaam.Tukafika nyumbani kwangu na nikawakaribisha na sote tukaingia ndani kuingia ndani
"Ehe sir Eddy umejitahidi?"
Rahma ni muongeaji sana kiasi kwamba hakuwa anampa mwenzake nafasi, ya kuzungumza na mimi japo hata kuchangia mada ya jambo tunalo lizungumzia
"Nimejitahidi vipi?"
"Chumba chako ni kizuri"
"Asante"
"Sir acha sisi twende tutakuja kukutembelea jumamosi"
"Sawa karibuni"
Wakaondoka na kuniacha nikiendele na shughuli zangu za kawaida, ikiwemo kupika chakula cha mchana, nilicho kijumlisha na chakula cha usiku.Nikaendelea kufanya kazi kwa juhudi siku zote za kazi yangu, huku upendo wangu wa kuipenda kazi yangu ukizidi kuongezeka kadri ya siku zilivyozidi kukatika

Advertisement
==
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG