Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA
***ilipoishia***
wachawi
wachawi wenzake walimpokea kwa furaha...bi'chenda alizipiga hatu mpaka
kwa mkuu wa wachawi na kumkabidhi mtoto huyo mchanga sherehe kubwa
ikafanyika usiku huohuo....walicheza ngoma za kichawi huku wakila nyama
za binadamu....ghafla mkuu wa wachawi akapaza sauti na
kusema,,"Tusikilizane......kijiji kizima kikawa kimya kisha akazipiga
hatua huku kambeba doto...akapanda na kusimama juu kwenye mgongo wa
binadamu waliyemchukuwa kichawi usiku huo kwaajili ya kumfanya jukwaa la
kumkuu wa wachawi..kisha akasema...........
***Endelea***
Siku
ya leo,,,ni siku ambayo itakuwa ni yenye baraka kubwa katika kijiji
chetu....mtoto huyu mchanga....ameteuliwa na miungu ya kuzimu....wachawi
wengine wakaanza kupiga makofi huku wakiongea Lugha ambayo haina maneno
ya kibantu..
(lugha
isiyokuwa rasmi.haieleweki)..kisha mkuu wa wachawi akachukua kisu
pamoja na sumu ya nyoka iliyochanganywa na dawa ya kichawi..akamchana
doto kiunoni kwa kutumia kisu hicho kisha..akachukua ile sumu ya nyoka
iliyochanganywa na dawa ya kichawi akampaka kwenye jeraha hilo
kililokuwa likitoa Damu....
kutokana
na maumivu makali Doto alilia kwa mfululizo bila kunyamaza....kisha
mkuu wa wachawi akamteuwa mwanamke mmoja aliyekuwa anamtoto
anayemnyonyesha miongoni mwa wachawi wa kijiji hicho..(GAMBOSHI)
akamkabidhi Ili awe anamnyonyesha Doto pamoja na kumlea... mlaka
atakapofikisha umri wa kuitumikia kazi ya miungu wa kuzimu rasmi..baada
ya kumaliza sherehe hiyo..wachawi walitawanyika,,,kila mmoja alipanda
kwenye ungo wake na kutoweka kimiujiza...
Bi'chenda
ajajitokeza chumbani mwake...akavua ile kaniki nyeusi..pamoja na irizi
zake mbili akaziweka kwenye kimkoba chake,,kisha akaweka ndani ya begi
na kufunga zipu ya begi..akapanda kitandani akaanza kuutafuta usingizi..
******************
asubuhi
palipokucha alionekana Rose akiwa ameketi kitandani huku macho
uamevimba kutokana na kulia usiku kucha....Rose hakuweza kabisa kuoata
usingizi usiku wa jana...Seba alikuwa na kazi kubwa ya kumbembeleza
mkewe usiku kucha...wlikesha bila kutarajia.....
ghafla
mlango wa chumbani ukagongwa......seba akanyanyuka,,akazipiga harua
kwenda kufungua mlango...... alipofungua alimuona mama yake Bi'chenda
akiwa amebeba beseni lililokuwa na maji ya moto ndani yake kwa ajili ya
kumkanda Rose sehemu zake za siri.... seba aliamua kutoka nje ya chumba
ili kumpisha mama yake akamkande mkwe wake..
Bi'chenda
alijifanya kumbembeleza rose akimsihi anyamaze huku akisema,,"nyamaza
mwanangu ni mipango ya Mungu...atakujalia utapata watoto tena usilie....
Rose alimtazama mama mkwe wake kwa huzuni huku akionekana kufarijika na
maneno hayo akasema"asante mama yangu...kisha akavua nguo na kulala
chali kitandani....bi'chenda akaanza kumkanda..
0 comments:
Post a Comment