Makamu wa rais wa zamani nchini Zimbabwe Joice Mujuru ameshambuliwa kwa mawe wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa siasa.
Chama
cha upinzani cha Mama Mujuru cha National People's Party kimesema Bi
Mujuru na wanachama wengine walishambuliwa kwa mawe walipokuwa wakifanya
mkutano wa kampeni katika viunga vya mji wa Harare.
Kwa
mujibu wa Shirika la Utangazaji BBC limesema kwamba msemaji wa chama
hicho ameweka wazi kwamba mama Mujuru amejeruhiwa kidogo huku taarifa
kutoka ndani ya chama ikisema watu wanane walijeruhiwa katika shambulio
hilo.
Taarifa ya chama hicho imesema shambulio hilo lilikuwa la kisiasa na lilifanywa na wanachama wa chama tawala cha Zanu-PF Party.
Kwa
upande mwingine Rais mpya wa nchi hiyo Emmerson Mnangagwa, ameahidi
kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini humo baadae mwaka huu na
kuuhakikishia umma wa nchi hiyo kwamba uchaguzi huo utakuwa huru na wa
haki.
0 comments:
Post a Comment