Home » » AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 87 na 88

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 87 na 88

Unknown | Tuesday, April 17, 2018 | 0 comments
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA                      
ILIPOISHIA  

Delifina alizungumza huku akisimama, nikatazama kwa mbali nikaona uwanja  wenye nyasi nzuri na kwa mbele kuna majengo yanayo waka taa.
“Hapa ndio ikulu?”  
“Ndio”
“Ni watu gani ambayo wanahitaji kukua?”
“Ni adui wa baba yangu, anaitwa Livna Livba na hii sio mara yake ya kwanza kuhitaji kuniua. Asante sana Dany na Mungu akubariki”
Delfina alizungumza akanibusu shavuni na kuondoka huku akikimbia. Taswira ya Livna amsaliti wangu ikaanza kunijia kichwani mwangu, nikajikuta nikitawaliwa na hasira kali na kwa haraka nikageuka na kuanza kurudi msituni huku nikikimbia, nikihitaji kumkamata mmoja wa watu wake nimpatie meseji atakayo ipeleka kwa bosi wake

ENDELEA
Ndani ya msitu mzima kazi yangu ni kuhakikisha kwamba ninawapata watu wa Livna Livba. Ila kadri nilivyo zidi kusonga mbele sikuweza kuona dalili yoyote ya mtu ndani ya huu msitu na nikajikuta nikitokea sehemu ya maegosho ya magari. Japo polisi na waandhishi wa habari walisha jitokeza kuchukua matukio ambayo yametokea katika hili eneo. Nikajipenyeza penyeza kwa watu ambao wamekusanyika pemebi wakitazama jinsi polisi wakifanya uchunguzi wao. Nikaanza kurudi kuelekea sehemu ambapo tulitokea kutoka kwenye ngome yetu ya Al-Shabab. Nikafanikiwa kufika salama pasipo mtu yoyote kuniona, nikawakuta Ruben na rafi yetu ambaye tulitoroka naye.

“Dany ulikuwa wapi?”
“Babu pale lile tukio lilivyo tokea, nilijibanza kwenye moja ya kona ndio muda huuu ndio ninatoka baada ya kuona mambo kutulia”
“Ahaa ilikuwa bado nusu tuingie kwa maana tulihisi ni miongoni mwa watu walio kufa”
“Ahaaa sifi  kirahisi namna hiyo”
Sikutaka marafiki zangu kuweza kufahamu kwamba kuna jambo gani ambalo nimelifanya. Tukaingia kwenye shimo letu, tukachukua tochi zetu, tukaziwasha na kuelekee sehemu ambayo inatokezea katika chumba kilichopo ndani ya ngome hii. Hatukuchukua muda sana tukafika kwenye shimo letu, akapanda mmoja mmoja. Tukafunika sehemu hii tunayo tokelezea, chumba tukakipanga vizuri, nikabadilisha nguo zangu na kuvaa nguo nilizo kuwa nimezivaa.

“Sasa waskaji?”
“Poa bwana Dany japo mambo yameharibika”
“Musijali, mukipata nafasi nyingine kama hii musisahau kunialika”
“Usijali kaka, sisi kila weakend tunatoka”
“Poa poa”
Nikafungua mlango na kutoka kaatika chumba hichi. Japo ni majira ya usiku sana ila nikajitahidi kutembea kwa kujiamini kama nipo kwenye lindo. Nikafanikiwa kufika chumbani kwangu, nikaingia, nikawasha taa kuangalia  kama usalama wa chumba kipo, kisha nikaizima na kulala kitandani. Sura ya Livna Livba kwa mara kadhaa ikaanza kunitawala kichwani mwangu, kila muda ninajaribu kufikiria ni jinsi gani ninavyo weza kumpata.

‘Au  atakuwepo hapa Somalia?’
Nilijiuliza maswali mengi. Matumaini yakaanza kunijaa moyoni mwangu kwa maana tayari nimesha gundua njia ambayo inaweza kunisaidia kutoka katika hii kambi pasipo watu wengine kunistukia, kumshuhulikia Livna Livba kisha nitafwatia na K2 hawa ndio wanawake ambao ni maadui zangu wakubwa chini ya hili juu. Hadi kuna pambazuka kichwa changu kimesha panga mipango ya kipelelezi ya chini chini, kuhakikisha ninampata adui yangu mmoja baada ya mwengine.

“Ni muda wangu sasa”
Nilizungumza huku nikijinyoosha viungo vyangu, nikaanza kufanya mazoezi madogo madogo ndani ya chumba changu. Nilipo hakikisha nipo vizuri, ndio nikatoke nje kuelekea kwenye mazoezi ya kikundi.
“Jana usiku ulikuwa wapi?”
Mwalimu wangu wa mazoezi aliniuliza kwa sauti ya chini sana pasipo mwajeshi mwengine kusikia. Kidogo nikastuka ila akili yangu sasa hivi nimesha iweka katika hali ya kuweza kupanga na kupangua matatizo kwa ustadi wa hali ya juu.
“Nilikuwa kwa Ruben”


Advertisement
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG