Mtu
mmoja nchini Uganda anayejulikana kwa jina la Moses Okello amehukumiwa
kifungo cha nje na kufanya kazi za jamii kwa siku 40, baada ya kukutwa
na hatia ya kumtilia pilipili mke wake kwenye nguo ya ndani.
Mke
wa Okello aliiambia mahakama kuwa mume wake huwa anapenda akiwa amevaa
nguo hiyo, na siku hiyo alimlazimisha sana kuivaa na kutekeleza, na
baada ya muda mfupi alihisi kuwashwa na kuvimba sehemu za siri na kuamua
kwenda kumuona daktari, ndipo walipogundua ilikuwa ni pilipili.
“Aliniambia
anavutiwa sana na mimi nikiwa nimevaa hiyo nguo akawa ananilazimisha
kuivaa, baada ya kuivaa nikaanza kuhisi muwasho sana, nikaenda kumuona
daktari na kugundua ilikuwa pilipili”, amesema Mke wa bwana Okello
ambaye jina lake limehifadhiwa.
Moses alikiri kufanya tukio hilo kwa mkewe, na kusema kwamba ulikuwa ni utani ambao amezoea kufanyiana na mke wake huyo kipenzi.
0 comments:
Post a Comment