Basi
la abiria mali ya kampuni ya Tahmeed coach linalofanya safari zake kati
ya Dar es Salaam kwenda nchini Kenya jijini Mombasa limepinduka leo na
kusababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi watu wengine zaidi ya 20.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema
kuwa basi hilo limepinduka katikati ya Msata na Kabuku mkoani katika
eneo la Kitumbi Tanga na kudai kuwa mtu mmoja alifariki hapo hapo huku
wengine zaidi ya 20 wakijeruhiwa.
"Ni
kweli ajali imetokea imesababisha kifo cha mtu mmoja na kujeruhi
wengine 20, majeruhi wengine walipata majeraha madogo madogo hivyo
tayari wamesharuhusiwa lakini majeruhi wengine watano nado wanapata
matibabu"
Hii
ni ajali ya pili kwa mwaka huu inayohusisha basi za Tahmeed kutokea
katika eneo la Kitumbi, Januari 29, 2018 basi jingine liliwaka na
kuteketea kwa moto katika kijiji cha Kitumbi wilayani Handeni mkoani
Tanga.
0 comments:
Post a Comment