Mtuhumiwa
namba moja ambaye anahusishwa na kifo cha msanii muziki nchini Uganda,
Mowzey Radio amekamtwa na Jeshi la Polisi nchini humo.
Kijana
Wamala Godfrey mwenye umri wa miaka 28 ndiye alikuwa akisakwa na polisi
kama mtuhumiwa mkuu mara baada ya mmiliki wa bar, Egesa George na
Meneja wake kilipotokea kifo cha Radio kushikiliwa na Polisi.
Wamala alikamatwa katika eneo la Kyengera alipokuwa amejificha kwa siku
kadhaa nyumbani kwa rafiki yake. Wamala amehamishiwa mjini Entebbe.
Mwimbaji Mowzey Radio alifariki dunia Februari Mosi mwaka huu kutokana
na majeraha ambayo aliyapata kichwani kufuatia ugomvi katika bar hiyo.
Kamanda wa Polisi Kampala, CP. Frank Mwesigwa amethibitisha kushikiliwa
kwa Wamala Godfrey na kueleza kuwa kwa sasa wanaandaa majalada ili
kuweza kumfikisha mahakamani.
0 comments:
Post a Comment