Hayo
yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa
Polisi Mohamed .R. Mpinga wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa
habari na kusema mnamo Februari 3, 2018 kwa kushirikiana na viongozi wa
hospitali hiyo walifanikiwa kumshika kijana huyo aliyefahamika kwa jina
la Happy Charles (24) ambae anajishughulisha na kazi ya Mama lishe.
Aidha,
Kamanda Mpinga amesema mnamo Februari mosi mwaka huu majira ya saa 4:00
usiku katika wodi ya watoto Hospitali ya Mkoa wa Mbeya iliyopo Kata ya
Forest Mpya, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya, mwanamke mmoja
anayefahamika kwa jina la Sarah Mwasanga Mkazi wa Iganzo akiwa katika
wodi ya wazazi Hospitalini hapo baada ya kujifungua mtoto wa kike
aligundua kuibiwa kwa mtoto huyo na mtu asiyefahamika.
Kutokana
na tukio hilo, uongozi wa Hospitali hiyo ulitoa taarifa kituo kikuu cha
Polisi na ndipo upelelezi kuhusiana na tukio hilo ulianza kufanyika.
Msikilize
hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi Mohamed
.R. Mpinga pamoja na mzazi wa aliyeibiwa mtoto wakifafanua vizuri juu ya
tukio hilo.
0 comments:
Post a Comment