Home » » "Kamateni wote" - Mwigulu

"Kamateni wote" - Mwigulu

Unknown | Monday, February 05, 2018 | 0 comments
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amelitaka jeshi la polisi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa na kwamba taasisi hiyo ndiyo inayoshughulika na haki za watu na wasipofanya kwa uadilifu yapo madhara makubwa kwa jamii na kutoka kwa wahalifu

Akizungumza  katika uzinduzi wa ujenzi wa Kituo cha polisi Wilaya ya Pangani leo, Dk Mwigulu amesema kuwa wilaya ya Pangani ni lango ambalo wahalifu hasa wahamiaji haramu hupitia kwenda kusini mwa Tanzania. 
‘’Kamateni wahalifu wote wanaoingia kimagendo au wanaoingiza mizigo kimagendo hakuna mjadala kamateni na wafikisheni katika vyombo vya sheria ,’’amesema Dk Mwigulu.
Kwa mujibu wa Dk Mwigulu, Mikoa ya kaskazini mwa Tanzania inaongoza kwa kuingiza wahamiaji haramu na bidhaa kwa magendo kwasababu ipo mipakani hivyo kuamua kuchangia vifaa vya ujenzi ili kuunga mkono juhudi hizo.
‘’Ujenzi huu wa kituo cha polisi utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama zaidi hivyo mimi nitachangia nondo 150 baada ya mifuko 450 ya cement kupatikana basi ujenzi uanze haraka iwezekanavyo na kituo kiwe cha hali ya juu kikubwa.’’ amesisitiza
Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi wilaya hiyo, Mrakibu Mwandamizi wa polisi Christina Musyani amesema kuwa wilaya hiyo ina vituo vitatu pekee vya polisi ambavyo havitoshi na mazingira yake hayaridhishi.
Amesema wameamua kuanza ujenzi wa kituo hicho ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wakazi wa eneo hilo ambao kwa sasa hulazimika kusafiri umbali mrefu kutafuta vituo vya polisi.
"Kwa kushirikiana na wananchi, Mbunge na halmashauri tumeamua kuanza ujenzi wa kituo cha kisasa ,’’ amesema Christina.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG