Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia kifo cha Kingunge Ngombale Mwiru akisema historia itamkumbuka.
Akizungumza leo Februari 2, 2018 ameanza kwa kusema “namtakia mapumziko mema.”
Amesema
Mzee Kingunge alikuwa miongoni mwa wazee wenye historia kubwa na
alionyesha ujasiri mkubwa wa kuhama chama chake cha CCM bila kuhofia
kuhudhuriwa kutokana na mazingira yalivyokuwa.
“Ni
mmoja wa wazee walioonyesha ujasiri mkubwa katika mazingira ya siasa za
Tanzania yalivyokuwa, akahama chama tena CCM bila hofu za kuhudhuriwa
akaeleza madhabi yake kuwa hiki chama (CCM) kinatupeleka kuzimu,”
amesema Lissu na kuongeza “historia itamkumbuka.”
Kingunge
aliyekuwa kada wa CCM mwenye kadi namba nane, Oktoba 4, 2015 alitangaza
kukihama chama hicho na kusema hatojiunga na chama chochote lakini mara
kadhaa alionekana akipanda majukwaa ya upinzani kumnadi aliyekuwa
mgombea urais wa Chadema/Ukawa, Edward Lowassa kwenye uchaguzi mkuu
uliofanyika Oktoba 25, 2015..
0 comments:
Post a Comment