Bado
inaonekana swala la Diamond Platnumz kudaiwa kulala na wasichana
wengine nyumbani kwake Madale, mama watoto wake Zari The Boss Lady
hajaichukulia poa na inadaiwa kuwa amekasirishwa na tuhuma hizo
zilizosambaa katika mitandao ya kijamii.
Diamond
siku kadhaa zilizopita alidaiwa kupeleka msichana mwingine na kulala
nae nyumbani kwake Madale, ila baada ya kuenea kwa video clip
ikimuonesha msichana huyo akiwa Madale, Zari alionesha kukasirishwa na
kuandika snapchat “Ati Madale State lodge au Madale Guest house?”
Baada
ya siku kadhaa kupita baadhi ya mashabiki waliamini inawezekana swala
hilo limepita ila comment ya Zari katika post ya instagram ya mama
Diamond inaonesha amekasirika bado, hiyo ni baada ya ku-coment katika
picha ya Mama Diamond aliyopost na kuandika “Kubwa la maadui”
ikimuonesha Mama Diamond akiwa Madale lakini Zari akacomment “Fanya tuhame Guest House tumuachie mwanao”
0 comments:
Post a Comment