Home » » Christian akamatwa na Cocaine pipi 59 uwanja wa ndege Dar

Christian akamatwa na Cocaine pipi 59 uwanja wa ndege Dar

Unknown | Monday, January 29, 2018 | 0 comments
Polisi Kikosi cha Viwanja vya Ndege jijini Dar es Salaam linamshikilia raia wa Nigeria akituhumiwa kupatikana na dawa za kulevya aina ya Cocaine.

Christian Ugbechi (26), anadaiwa kukamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kwa Julius Nyerere (JNIA) akiwa na pipi 59 zenye uzito wa zaidi gramu 800.

Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Matanga Mbushi amesema leo Jumatatu Januari 29,2018 kuwa mtuhumiwa anaishi na kufanya kazi nchini Ufaransa.

Amesema alikuwa akisafirisha dawa hizo za kulevya kwenda nchini Ufaransa.

"Tumemkamata mtuhumiwa akiwa na pipi 59, kati ya hizo 56 alizificha kwenye soksi na tatu amezitoa leo kwa njia ya haja kubwa. Yupo chini ya uangalizi maalumu,” amesema Mbushi.

Advertisement
==
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG