Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limesema mitihani ya kuhitimu kidato cha sita itaanza Mei 7 hadi 24, 2018.
Kwa
mujibu wa ratiba iliyotolewa na Necta Januari 26, 2018 inaonyesha somo
la kwanza litakuwa ni masomo ya jumla ‘General Studies’ na somo la
mwisho litakalofanyika Mei 24 litakuwa ni Baiolojia 3C (kwa vitendo).
Msemaji
wa Necta, John Nchimbi amesema “lengo la kutoa ratiba ni kuwafanya
wanafunzi na walimu wao kujiandaa kwa ajili ya mitihani yao.”
“Ratiba
inawasaidia wao kuweza kufanya maandalizi lakini kuwaweka sawa
kisaikolojia na kujua mitihani ipo, itakuwa lini hadi lini na muda
gani,” ameongeza
0 comments:
Post a Comment