Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameitaka
TFF kuyafanyia kazi malalamiko yote yanayohusu michezo ya ligi daraja
la kwanza, kati ya Dodoma FC vs Alliance na Pamba vs Biashara.
Sakata
la maamuzi yasiyo ya haki katika michezo ya Dodoma FC dhidi Alliance ya
Mwanza na Pamba ya Mwanza dhidi Biashara ya Musoma ndio limefanya
Waziri mwenye dhamana ya michezo kutoa agizo hilo kwa shirikisho ili
kuhakikisha utata huo unamalizika.
Katika
taarifa yake Waziri Mwakyembe ameeleza kusikitishwa na malalamiko ya
vitendo vya uonevu na upendeleo katika maamuzi ya mechi hizo huku TFF
ikiwa kimya bila kutoa ufafanuzi wa maamuzi hayo.
Mechi
hizo zilipigwa Disemba 30 maamuzi yake kugubikwa na utata mkubwa hivyo
Waziri amemtaka Rais wa TFF Wallace Karia na viongozi wengine wahusika
kuchukua hatua za kuchunguza maamuzi hayo na kuchukua hatua
.
.
0 comments:
Post a Comment