WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bibi Anna
Mghwira asitishe uuzwaji wa mali za Chama cha Ushirika cha Kilimanjaro
(KNCU).
Ametoa
agizo hilo jana jioni (Jumatano, Januari 17, 2018) wakati akihutubia
wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa
Serengeti, wilayani Tarime.
Hatua
hiyo imekuja baada ya KNCU kutangaza kuuza shamba lake kwa ajili ya
kuiwezesha benki yake ya KCBL kutimiza sharti la mtaji la Benku Kuu ya
Tanzania (BoT).
Benki
hiyo ya KCBL inatakiwa kutimiza sharti la kuwa na mtaji kamili
unaotosha wa shilingi bilioni tano (5) katika kipindi cha miezi sita
tangu kutolewa kwa tangazo hilo.
Waziri
Mkuu alisema ni marufuku kuuza mali za Ushirika huo, hususan katika
kipindi hiki ambacho Serikali inafanya uhakiki wa mali za vyama
mbalimbali vya Ushirika nchini.
Alisema
Serikali imedhamiria kuimarisha Ushirika nchini na sasa inafanya
uhakiki wa mali za vyama vya Ushirika na watakaobainika kuhusika na
ubadhilifu watachukuliwa hatua.
Januari
4, 2018 BoT ilizipa miezi sita benki tatu ili ziweze kuongeza kiwango
cha mtaji unaohitajika kutokana na matakwa ya kisheria ya kuwa na mtaji
kamili wa kutosha.
Benki
hizo ni Kilimanjaro Co-Operative Bank Limited, Tanzania Women Banki Plc
na Tandahimba Community Bank Limited, zitakaposhindwa kutekeleza agizo
zitachukuliwa hatua.
BoT
ni itazifutia leseni na kusimamisha shughuli za kibenki chini ya
ufilisi, iwapo benki hizo zitashindwa kutekeleza agizo hilo ihadi
kufikia Juni 30, 2018.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
0 comments:
Post a Comment