Transfoma iliyopata tatizo
Shule ya sekondari ya Lupalilo inakabiliwa na ukosefu wa nishati ya umeme
kwa zaidi ya mwezi mmoja hivi sasa baada ya Transfoma iliyokuwepo kuungua na
kusababisha kukwama kwa shughuli mbalimbali
shuleni hapo ikiwemo wanafunzi
kushindwa kujisomea usiku pamoja na
kuhatarisha usalama wa wanafunzi
baada kukosekana kwa nishati hiyo hasa nyakati za usiku
Akizungumzia Hali hiyo makamu mkuu wa shule
Mwalimu LUNANILO KILATU amesema ni zaidi ya mwezi mmoja sasa wamekosa nishati hiyo baada ya transfoma
kuungua na kupelekea baadhi ya shughuli
kukwama shuleni hapo ikiwemo wanafunzi kushindwa kujisomea nyakati za usiku
hivyo shule kulazimika kutumia jenereta ambalo amedai linawaongezea gharama
zaidi
Amesema wamesharipoti suala hilo kwa shirika la
umeme TANESCO wilaya ya Makete tangu lilipotokea lakini hadi sasa ufumbuzi
haujapatikana ingawa anaimani kuwa wanashughulikia
Kwa upande wa baadhi ya wanafunzi shuleni hapo
waliozungumza na mwandishi wetu wamesema wanakumbana na changamoto nyingi baada
ya kukosekana nishati hiyo ikiwemo kushindwa kujisomea nyakati za usiku huku
wakihofia juu ya usalama wao hususani wanafunzi wa kike
Hata hivyo Tumemtafuta Meneja wa Tanesco
wilaya ya Makete Ndugu HENRIKO RENATUS
kupata ufafanuzi ambapo amesema mpaka sasa wanasubiri Transfoma nyingine
kwani wameshatuma maombi ya kuomba transfoma na pindi zitakapowasili wataipa
kipaumbele shule hiyo kutokana na uhitaji
Ni zaidi ya mwezi sasa shule hiyo ikabiliwa na tatizo hilo la ukosefu wa umeme na kukwamisha mambo mengi pamoja na usalama wa wanafunzi kuwa mdogo na kupunguza uwezekano wa wanafunzi kujisomea nyakati za usiku kama ilivyokuwa awali
Mwanafunzi wa Lupalilo Sekondari akizungumza na mwandishi wetu
Muonekano wa shule ya Lupalilo Sekondari
0 comments:
Post a Comment