Na Kadama Malunde
Jeshi
la polisi mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata silaha ya kivita aina
ya AK-47 iliyotupwa na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi waliokuwa
wanataka kuvamia kiwanda cha kutengeneza mafuta ya kupikia cha Jielong
Holdings (Tanzania) Ltd kilichopo Nhelegani katika kata ya Kizumbi
manispaa ya Shinyanga.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari leo Alhamis Januari 18,2018 Kamanda wa
polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule amesema walikamata silaha hiyo
usiku wa kuamkia leo majira ya saa tano eneo la Tinde wakati majambazi
hao wanafuatiliwa na polisi ndipo wakaamua kutupa bunduki hiyo.
“Silaha
hii aina ya AK-47 yenye namba 18116428 ilikuwa imefungwa kwenye skafu
yenye rangi ya nembo ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
ikiwa na risasi 25 ndani ya magazine yake na risasi zingine 8,zikiwa
kwenye mfuko mdogo wa nailoni,” alieleza Kamanda Haule.
“Majambazi
wawili pia walitelekeza pikipiki aina ya SANLG yenye namba za usajili
MC 856 BPF,mafuta ya cherehani ya kulainishia silaha,tochi mbili na koti
zito,” aliongeza.
Alisema
jeshi la polisi lilipata taarifa za majambazi hao kutaka kuvamia
kiwanda hicho kinachomilikiwa na raia wa China tangu tarehe 6.01.2018
kisha kuanza kuwafuatilia na kubaini kuwa baadhi yao ni wakazi wa Kahama
na Ushirombo ambapo amewataka kujisalimisha polisi.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha silaha aina ya
AK-47 yenye namba 18116428 na mafuta ya kulainishia silaha yaliyotupwa
na majambazi waliotaka kuvamia kiwanda cha Jielong
Bunduki
aina ya AK-47 yenye namba 18116428 iliyokuwa imefungwa kwenye skafu
yenye rangi ya nembo ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
iliyotelekezwa na majambazi waliotaka kuvamia kiwanda cha Wachina mjini
Shinyanga
Silaha na vifaa vilivyotelekezwa na majambazi
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha skafu iliyotumika
kufunga bunduki aina ya AK-47 yenye namba 18116428
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha bunduki aina ya
AK-47 yenye namba 18116428 iliyotupwa na majambazi waliotaka kuvamia
kiwanda cha Jielong
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha risasi zilizotelekezwa na majambazi
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Simon Haule akionesha pikipiki aina ya
SANLG yenye namba za usajili MC 856 BPF iliyotelekezwa na majambazi
0 comments:
Post a Comment