WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemkabidhi Mhandisi wa Maji wa Halmashauri ya
wilaya ya Rorya, Mhandisi Obetto Sasi kwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais-TAMISEMI, Bw. Josephat Kandege baada ya kutoridhishwa na utendaji
wake.
Ametoa
uamuzi huo jana jioni (Jumanne, Januari 16, 2018) wakati
aliposimamishwa na umati wa wananchi kwenye mji Mdogo wa Shitari
alipokuwa njiani kuelekea kwenye kijiji cha Bubombi wilayani Rorya.
“Hatuwezi
kuwa na mtumishi wa aina hii ambaye kila eneo tunakutana na changamoto
za maji huku kukiwa hakuna hatua zinazochukuliwa licha ya Serikali kutoa
fedha, hivyo namuagiza Katibu Tawala wa Mkoa alete mhandisi mwingine wa
maji.”
Pia
Waziri Mkuu amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Profesa Kitila Mkumbo kwenda wilayani Rorya na kukagua mradi wa maji
katika mji Mdogo wa Shirati na kuona namna ya kuutekeleza.
Amesema
kwa sasa Serikali inatekeleza Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya
kumtua mama ndoo. Kampeni hiyo inalenga kuwaondolea wananchi tatizo la
upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama, hivyo itawachukulia hatua
wote watakaokwamisha miradi ya maji.
Awali,
Mkuu wa Mkoa wa Mara Bw. Adam Maliwa alimueleza Waziri Mkuu kwamba
changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika mkoa
huo inatokana na watendaji wa idara hiyo kutokuwa na uwezo wa kutosha
kiutendaji.
Wilaya
ya Rorya inatekeleza miradi 11 ya maji ya bomba kupitia Programu ya
Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RWSSP) katika vijiji vya Kinesi,
Randa, Utegi, Mika,Kirogo, Nyihara, Kisumwa,Nyamkonge, Nyambori,
Gabimori na Marasibora.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
0 comments:
Post a Comment