Upande
wa mashtaka katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Agnes
Gerald maarufu kama ‘Masogange’ umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, kuwaonya upande wa utetezi kwa kushindwa kutoa ushahidi wao
kwa mara ya tatu mfululizo.
Hatua
hiyo imekuja baada ya wakili wa utetezi, Nehemia Nkoko kudai mbele ya
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri kuwa wakili mwenzake, Reuben
Simwanza ndiye aliyeandaa mashahidi na kwamba ameshindwa kutokea kwa
kuwa anaumwa.
Wakili
wa Serikali, Constantine Kakula alitaka upande huo uonywe leo Jumatano
baada ya shauri hilo kufikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kuendelea
na ushahidi.
Kutokana
na hali hiyo, Wakili Nkoko amesema atahakikisha anaandaa mashahidi ili
itakapotokea wakili mmoja hayupo, mwengine aendelee na shauri.
"Hatuna
pingamizi na sababu zilizotolewa na upande wa utetezi lakini tunaomba
Mahakama itambue kuwa ni mara ya tatu kwa upande wa utetezi inaahirishwa
kesi hii? Amesema wakili wa Kakula na kuongeza;
"Mawakili
wapo wengi lakini wanashindwa kuendelea kutoa ushahidi wao wa upande wa
utetezi basi kama hawawezi, waache mshitakiwa aendelee na kesi
mwenyewe."
Kutokana na hali hiyo, upande wa mashtaka umeomba ahirisho la mwisho kwa sababu kesi ni ya muda mrefu.
Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 26, mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa.
Masogange
ataanza kujitetea baada ya Mahakama kumkuta na kesi ya kujibu baada ya
kusikiliza mashahidi watatu wa upande wa mashitaka.
0 comments:
Post a Comment