Watuhumiwa
katika kesi ya matukio mbalimbali ya ugaidi mkoani Arusha, Leo January
16, 2018 wamevua nguo na kubaki utupu wakati wakishushwa kwenye basi la
Magereza la Kisongo walipofikishwa katika Mahakama ya hakimu mkazi
Arusha.
Baadhi
ya watuhumiwa wamefikia uamuzi huo wakidai kuchoshwa na hatua ya
kufikishwa Mahakamani na kusomewa mashtaka kisha kurejeshwa mahabusu
bila kesi yao kuanza kusikilizwa, jambo linalowalazimu kukaa mahabusu
kwa zaidi ya miaka minne bila shauri lao kusikilizwa.
Mapema
leo, mahabusu hao walifikishwa Mahakamani wakiwa kwenye basi la
magereza na kuamuriwa kuteremka, lakini baadhi yao waliteremka wakiwa
hawana nguo na kutembea kuelekea zilipo mahabusu za Mahakama hiyo jambo
lililowafanya wananchi waliokuwepo eneo la Mahakama kupata taharuki.
Kabla
ya kufanya tukio hilo mahabusu hao wamekuwa wakilalamika katika
Mahakama hiyo juu upelelezi kucheleweshwa katika shauri lao, wameiomba
Mahakama imwamuru Mwanasheria wa Serikali kuharakisha upelelezi wa
shauri lao kwa sababu limekuwa la muda mrefu na wao wakiendelea kuumia
mahabusu.
Shauri
hilo leo lilikuja kwa ajili ya kutajwa na Hakimu Patricia Kisinda wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, ameahirisha shauri hilo kutokana na
upelelezi kutokamilika hadi January 30, 2018.
Watuhumiwa hao wamerejeshwa mahabusu katika gereza kuu la Kisongo chini ya ulinzi mkali wa askari wa magereza.
April
25 mwaka jana baadhi ya mahabusu hao waligoma kushuka kwenye gari la
Magereza jambo lililoilazimu Mahakama hiyo kuhamia nje na kuwasomea
mashtaka na kisha kurejeshwa Mahabusu wakiwa chini ya ulinzi mkali.
0 comments:
Post a Comment