Mbunge
wa Chemba kwa tiketi ya CCM, Juma Nkamia amefunguka na kusema amemsikia
Rais kuhusu kutohitaji kufanya mabadiliko ya Katiba na kubadili ukomo
wa Urais na kudai Rais mwenyewe hawezi kusema anataka kuendelea kuongoza
bali watu ndiyo hupelekea hilo.
Juma
Nkamia amesema hayo wakati akiongea na kituo kimoja cha habari cha
Kimataifa na kudai kuwa ametafakari kauli ya Rais Magufuli na kuomba
ushauri kutoka kwa watu na mwisho kusema kuwa yeye haoni tatizo Rais
kubadili ukomo wa Rais kutoka miaka 5 mpaka 7 hivyo atazungumza na Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai
"Mhe.
Rais ambaye ni Mwenyekiti wa chama changu amesema yeye asingependa na
hafurahishwi na hilo jambo sasa mkubwa akishasema wewe uliopo chini
unatafakari hoja yako kwanza na unapata ushauri pia lakini mimi
nakubaliana na hoja yake. Ila siyo yeye anayetaka kuendelea, mimi kwa
mtazamo wangu na kwa kazi anazofanya na nikipita katika maeneo mengi
wananchi wanaridhika na utendaji wake na siku zote haiwezekani Rais
mwenyewe akasema mimi nataka kuendelea, bali ni wale ambao tunamuangalia
utendaji wake wa kazi ndiyo wanaweza kutoa mapendekezo" alisema Nkamia
Mbunge
huyo alizidi kusisitiza kuwa "Mimi niseme kwamba sisi wananchi pamoja
na mimi na nafasi yangu kama Mbunge na kwa mujibu wa Kanuni na taratibu
za Bunge ninaona kwamba Mhe. Rais kubadilisha miaka mitano kwenda saba
si jambo la ajabu sana. Hivyo kwa mujibu wa kanuni za Bunge nitazungumza
na Mhe. Spika na maelekezo ambayo nitapewa na Spika wa Bunge
nitayafanyia kazi" alisema Nkamia
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mnamo tarehe 13 Januari, 2018
alifunguka na kuweka wazi kuwa haridhishwi na hapendi mjadala uliokuwa
ukiendelea kuhusu kufanya mabadiliko ya Katiba na kuongeza ukomo wa
uongozi kutoka miaka mitano ya sasa na kwenda miaka saba.
0 comments:
Post a Comment