Home » » Watu saba wamekufa huko Ethiopia kaskazini

Watu saba wamekufa huko Ethiopia kaskazini

Unknown | Monday, January 22, 2018 | 0 comments

Watu saba wamekufa huko Ethiopia kaskazini baada ya vikosi vya usalama kufyatua risasi kwenye mkusanyiko wa watu waliohudhuria tamasha la kidini siku ya jumamosi.
Vifo hivyo katika mji wa Waldiya vimesababisha maandamano ya siku mbili yaliyosababisha uharibu wa nyumba, magari na barabara kufungwa .
Mashuhuda wanasema shida ilianza siku ya jumamosi pale waumini hao walipoanza kuimba nyimbo za kuipinga serikali na ndipo vikosi vya serikali vilianza kuwafyatulia risasi na kusababisha majeraha na vifo.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG