Home » » Serikali yatoa Msimamo wake kwa Klabu ya Simba kuhusu suala la uwekezaji

Serikali yatoa Msimamo wake kwa Klabu ya Simba kuhusu suala la uwekezaji

Unknown | Monday, January 22, 2018 | 0 comments
Na Anitha Jonas – WHUSM
Dar es Salaam
Serikali imetoa msisitizo kwa Klabu ya Mchezo ya Simba kuzingatia sheria na kanuni zinayosimamia suala la uwekezaji kwa Klabu zilizoanzishwa na wanachama ambapo wanachama wanachukua 51% na mwekezaji anachukua 49%.

Msisitizo huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipokutana na uongozi wa Klabu ya Simba na kuzungumza nao kufuatia kutoa asilimia 50% kwa mwekezaji wa klabu hiyo Bw.Mohamed Dewji waliyemtanganza hivi karibuni ambapo ni kinyume na sheria.

“Kanuni zinazosimamia masuala ya udhamini kwa vilabu zilifanyiwa marekebisho Novemba  2017 kwa ambapo ilioneka ni vyema klabu za michezo zilizoanzishwa na wanachama wanapopata muwekezaji basi mwekezaji achukue 49% na wanachama kutoka na mchango wao kwa mkubwa kwa klabu hiyo basi wapewe 51% lengo ikiwa ni mwanachama aweze kunufaika vizuri,”Dkt.Mwakyembe.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari Mheshimiwa Mwakyembe alisema kuwa serikali ya awamu ya tano hajaja kuuwa michezo bali lengo lake ni kuboresha michezo na kuifanya kuwa na tija zaidi pamoja na kuleta maendeleo endelevu katika sekta hiyo.

Naye Katibu wa Baraza la Michezo Taifa Bw.Mohamed Kiganga alieleza kuwa ofisi yake ipo katika maandalizi ya kuwaandikia barua Klabu ya Simba ya wapamsisitizo wa Serikali katika kuzingatia sheria katika suala la udhamini na barua hiyo itawafikia wiki ijayo.

Kwa Upande wa Kaimu Rais wa Klabu ya Simba Bw.Salim Abdallah alieleza vyombo vya habari kuwa wanashukuru serikali kwa kuwaeleza kuwa milango iko wazi pale watakapo kuwa na tatizo au watakapo hitaji ushauri wanaweza kuonana na watendaji wake.

Advertisement
==
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG