Rais
wa Marekani, Donald Trump amekana kuzitolea nchi za Afrika lugha chafu
katika kikao kilichofanyika Ikulu, kuhusu sera ya uhamiaji ya DACA.
Trump
alinukuliwa akitoa lugha ya matusi kwa nchi za Afrika akihoji kwanini
wanawahitaji Waafrika nchini kwao na kwamba ni bora wangeruhusu zaidi
watu kutoka Norway.
“Kwanini
tunataka watu hawa wote kutoka Afrika waingie hapa? Ni watu kutoka nchi
chafu (sh*thole countries)… tungekuwa na watu wengi zaidi kutoka
Norway,” tafsiri isiyo rasmi ya nukuu ya Trump.
Hata
hivyo, Trump ametumia mtandao wa Twitter ambako alishambuliwa vikali,
kujitetea kuwa hakutamka maneno hayo kwenye kikao hicho ingawa amekiri
kutumia maneno makali.
“Maneno
niliyotumia kwenye kikao cha DACA yalikuwa magumu, lakini hiyo sio
lugha niliyoitumia. Kilichokuwa kigumu zaidi kutoka kwangu ni kukataa
pendekezo la kuirudisha sera ya DACA,” tafsiri ya tweet ya Trump.
DACA
ni sera ambayo inawalinda vijana wadogo kupata nafuu katika taratibu za
uhamiaji nchini Marekani, na kuwalinda zaidi kutofukuzwa kirahisi.
Trump aliiondoa sera hiyo mwaka jana.
Mtandao
wa Twitter uligeuka kaa la moto kwa Trump baada ya habari hiyo
kuripotiwa na hasa watu kutoka Afrika ambao walianzisha hashtag na
kujaribu kumuonesha uzuri wa Afrika.
0 comments:
Post a Comment