Waziri
mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Fredrick Sumaye
amesema wanaojiuzulu ubunge na udiwani kwa kushawishiwa kwa fedha na
madaraka wanapaswa kukemewa na watu wote.
Katika
mahojiano na kituo cha habari za Azam Two jana Ijumaa Sumaye alisema
mwanasiasa anayefanya hivyo ni fisadi mkubwa kwani anachezea fedha za
wananchi wanazolipa kama kodi.
"Mtu
akijiuzulu kwa sababu za msimamo binafsi hiyo ni sawa lakini akijiuzulu
kwa nguvu ya fedha na madaraka tunapaswa wote kukemea,"alisema Sumaye.
Alihoji
uhalali wa mbunge kujiuzulu nafasi hiyo akiwa chama fulani na kuitaka
tena nafasi hiyo katika chama kingine kwa madai ya kutaka kuwatumikia
wananchi wakati hata huko alikojiuzulu alikuwa na uwezo wa kufanya
hivyo.
"Mtu
kama ni mbunge na aliwaomba kura wananchi ili kuwatumika anapaswa
kuwatumikia sio kuhama chama na kutaka tena ubunge kwani mbunge kazi
yake ni kuwasemea wananchi sio chama chake," amesema Sumaye.
0 comments:
Post a Comment