Deni
la zaidi ya shilingi milioni 800 ambalo lilikuwa likidaiwa na wakulima
wa Korosho kwa msimu wa 2016/2017 kwa vyama vya msingi (AMCOS) hatimaye
limelipwa.
Mwenyekiti
wa bodi ya chama kikuu cha ushirika cha Masasi, Mtwara Cooperative
Union (MAMCU) Joseph Kidando amesema tayari kiasi hicho cha fedha
kimeingizwa katika akaunti za vyama vya msingi kwaajili ya kugawanywa
kwa wakulima.
Aidha
mwenyekiti huyo amesema wamelazimika kulipa deni hilo kutokana na wao
kuwa walezi wa AMCOS na wakulima kwa ujumla na ametaja sababu za
kuchelewesha kulipwa kwa fedha hizo ni upotevu wa fedha uliosababishwa
na makosa ya viongozi wa AMCOS.
Kwa
upande mwingine Kidando ameeleza kuwa sababu nyingine kubwa
iliyosababisha upotevu wa fedha hizo ni kuingizwa kimakosa katika
akaunti tofauti za vyama vya msingi, ambapo baadhi ya viongozi
wasiowaaminifu waliamua kuzifanyia matumizi binafsi.
0 comments:
Post a Comment