Sekta
Binafsi nchini imekiri kuwa uhusiano kati yake na Serikali umezidi
kuimarika kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya uwekezaji na
ufanyajibiashara hapa nchini kuliko ilivyokuwa hapo awali na kwamba
hatua hiyo itachochea ukuaji wa uchumi wa nchi.
Kauli
hiyo imetolewa mjini Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta
Binafsi nchini (TPSF), Bw. Salum Shamte, wakati wa mkutano wa tatu kati
ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliojadili namna ya kukuza ushiriki wa
Sekta Binafsi katika kukuza uchumi wa viwanda nchini.
"Sekta
binafsi imenituma kuleta pongezi kwa Serikali inayoongozwa na
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo utambuzi wa kwamba Sekta Binafsi ni
mbia muhimu wa maendeleo ya Taifa letu" alisema Bw. Shamte.
Aliyataja
baadhi ya mafanikio yanayo onekana bayana kuwa ni pamoja na kuinusuru
Bandari ya Dar es Salaam kwa mabadiliko ya sheria ya fedha ya mwaka 2017
hasa kuondoa VAT kwenye biashara ya mizigo ya kimataifa na kuondokana
na umoja wa forodha ambao ulipunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha
biashara kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Bw.
Shamte alisema kuwa majadiliano hayo kati ya Serikali na Sekta Binafsi
kumeikoa sekta ya utalii hasa kwa kuondokana na kodi ya ongezeko la
thamani (VAT) kwenye leseni mbalimbali hatua ambayo imerejesha msisimko
wa sekta hiyo.
"Serikali
imepunguza pia mlolongo wa kodi kwa wakulima, japokuwa - kazi
haijakamilika lakini mwanzo ni mzuri" aliongeza Bw. Shamte
Alieleza
kuwa jitihada mpya na nzuri za kutatua changamoto za kodi kwa kampuni
zinazojihusisha na biashara kati ya Tanzania Bara na Visiwani, na kuanza
kufanya malipo kwa wakandarasi na watoa huduma wa ndani hatua ambayo
wanaamini itakuza matumizi ya ndani na mzunguko wa fedha.
Makamu
mwenyekiti huyo wa TPSF alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ni
sikivu na kwamba kwa mara ya kwanza, wanatarajia kushuhudia Bajeti Kuu
ya Serikali ya mwaka 2018/2019 ikiwa bora zaidi kwa kubeba mapendekezo
yao mengi yatakayosaidia kukuza sekta hiyo na pia kuboresha masuala ya
kodi na mapato ya Serikali.
Wakizungumza
kwenye mkutano huo, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, na
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage, wamesema
kuwa Serikali inathamini mchango wa Sekta Binafsi katika maendeleo ya
uchumi wa viwanda na kwamba itaendelea kutatua changamoto mbalimbali
zinazoikabili Sekta hiyo ikiwemo masuala ya kodi.
"Sekta
Binafsi ndiyo mhimili wa uchumi kwa hiyo ni muhimu tuhakikishe upande
wa Serikali tunafanya wajibu wetu kuiweesha Sekta hiyo iwe imara zaidi
na iweze kukua kwa sababu tutapata ajira, bidhaa bora na huduma
mbalimbali hatimaye kukuza uchumi wetu wa viwanda" alisisitiza Dkt.
Mpango
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji naye aliongeza kuwa Sekta Binafsi
ndiyo itakayojenga viwanda wakati Serikali itakuwa mwezeshaji ndio maana
wameamua kukaa pamoja kujadili changamoto zinazozikabili pande zote
mbili na kwamba baadae watajielekeza kujadili na kila Sekta ili
kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.
Wametoa
wito kwa Sekta binafsi nchini kujenga uaminifu na kufuata sheria na
kanuni za ufanyajibiashara na uwekezaji nchini ikiwemo kulipa kodi
stahiki.
Akizungumza
katika mkutano huo wa tatu uliojumuisha wadau mbalimbali kutoka ndani
na nje ya nchi, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID)
hapa nchini, Bw. Andy Karas, ameimwagia sifa Tanzania kwa kukuza uchumi
wake kwa wastani wa asilimia 7 na kushauri kuwa uchumi huo sasa
uelekezwe kutatua changamoto za wananchi hususan kukuza sekta ya kilimo
inayoa ajiri idadi kubwa ya watanzania.
Mwisho
0 comments:
Post a Comment