Mwanaharakati
na mwanamke shujaa nchini Tanzania, Joyce Kiria ameweka hadharani
kuhusu mahusiano yake kwa sasa na mumewe Henry Kileo ambaye alishawahi
kushika nyadhifa mbalimbali CHADEMA.
Joyce
Kiria amesema kuwa kwasasa mahusiano yake hayapo sawa kwani yeye
amekuwa ndiye baba na mama wa familia kwa kila kitu yaani kuhudumia
familia nzima pamoja na mumewe.
Akitoa
taarifa hiyo kwa umma kupitia ukurasa wake wa Instagram huku
akibubujikwa na majozi, Kiria amesema huwa anamshauri mumewe atafute
japo kazi itakayowaingizia kipato ili kusaidiana kutunza familia lakini
mumewe anakuwa mkali na kumpiga.
“Sikutegemea
kama ipo siku kwa mkono wako ungeunyanyua kunipiga (@kilewo2020mwanga)
ukasahau kabisa! ukasahau yooote. Nimeharibu career yangu kupigania
ndoto yako kwa kugawa watu wangu kwenye biashara zangu, nimepoteza ndugu
jamaa na marafiki, umeniachia nimebeba mzigo wa familia kwa muda wote,
Malipo yako ni kunipiga/ kunidhalilisha na kunitoa machozi, umenipiga
kwa sababu Mimi ni mnyonge siyo! sina nguvu, kwa sababu ni MWANAMKE Sina
nguvu za kupigana na MWANAUME. Umeniumiza mwili wangu unauma kila
mahali, ukanigongesha kwenye gari, ili iweje? Nia yako ilikuwa ni nini?
kuniua??,“ameandika Kiria huku akielezea jinsi alivyompigania mumewe
hadi kwenye kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2015 hadi akaingiza deni
kubwa na kufungiwa kipindi chake cha Wanawake Live kilichokuwa kinaruka
EATV.
“Haya
MACHOZI yangu namlilia Mungu wangu aliye juu, yeye ndo ataamua, kama ni
mimi niliandamana na watoto, nikakufanyia kampeni na deni kubwa
nikaingia mpaka nikafungiwa Kipindi hewami, ninakutunza wewe na Watoto
wako kwa miaka yote Mungu yupo. Leo umenipiga (@kilewo2020mwanga)?? Sawa
watakusifia hao wanaokusifu ujinga, wanaokuambiaga Mimi sikuheshimu,
badala wakwambie ufanye kazi utunze familia, Leo watakuona wewe ni
mwanaume kwa kunipiga.“amemaliza Kiria.
Mumewe
na Joyce Kiria ni moja ya vigogo wa CHADEMA na kwenye uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015 aligombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la Mwanga,
Kilimanjaro lakini kwa bahati mbaya alishindwa kupata nafasi hiyo.
Tazama video akielezea kwa hisia tukio hilo la kupigwa na mumewe;
0 comments:
Post a Comment