KATIBU
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Vincent
Mashinji amekanusha taarifa zinazosambaa mitandaoni kuwa, ni mgonjwa na
amelazwa katika Hospitali ya Amana.
Mashinji
amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote, yupo mzima wa afya na
anaendelea na kikao cha Kamati Kuu katika Hoteli ya Bahari Beach.
Amesema huenda kuna makosa kwa aliyemhusisha na kikao.
Taarifa hiyo ya uzushi iliyokuwa ikisambaa ilisema;
Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Dk. Vincent
Mashinji, ameugua ghafla na kukimbizwa katika Hospitali ya Amana jijini
Dar es Salaam.
Kaimu
Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Shani Mwaruka amethibitisha kumpokea
Dk. Mashinji leo saa tano asubuhi akiwa mahututi ingawa amesema ni
mapema mno kujua kinachomsumbua hadi hapo madaktari watakapotoa ripoti
baada ya kumfanyia uchunguzi.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amefika
hospitalini hapo kumjulia hali Dk. Mashinji ambaye amelazwa katika
chumba cha dharura.
0 comments:
Post a Comment