Jeshi
la Polisi mkoani hapa lilimshikilia na kumuachia kwa dhamana Mbunge wa
Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kwa tuhuma za kuratibu matukio
mawili ya kihalifu likiwamo la kuchoma nyumba aliyokuwa akiishi Katibu
wa Jumuiya ya Vijana wa CCM Iringa Mjini, Alfonce Muyinga.
Kamanda
wa polisi mkoani hapa, Julisu Mjengi amesema mbunge huyo alikuwa
akitafutwa kwa muda akituhumiwa kuratibu utekelezwaji wa matukio mawili
ya kihalifu likiwamo la Januari 17 la kuchomwa kwa nyumba aliyokuwa
akiishi Muyinga.
Mjengi
alitaja tukio la pili kuwa ni lile la Januari 15 la kubomolewa kwa
nyumba ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwangata Chadema, Anjelus Mbogo
aliyejizulu nafasi yake na kuhamia CCM.
"Mchungaji
Msigwa tulikuwa tukimtafuta kutokana na kuhusika kwake katika kuratibu
matukio mawili ya kihalifu, lile la Januari 15 la kubomoa nyumba ya
aliyekuwa diwani aliyehama Chadema na kujiunga na CCM pamoja na tukio la
kuchoma nyumba aliyokuwa akiishi Katibu wa Jumuiya ya Vijana wa CCM
Alfonce," amesema Mjengi na kuongeza;
"Na
jana (Jumatatu) amejisalimisha mwenyewe hivyo tumemhoji hadi majira ya
saa tatu usiku tulipomuachia kwa dhamana, taratibu nyingine zinaendelea
na tutawajulisha pindi tukapozikamilisha," amesema
Msigwa
amekuwa mtuhumiwa wa nne kukamatwa akihusisha na matukio hayo baada ya
wiki iliyopita jeshi hilo kueleza kuwa linawashikiliwa watuhumiwa watatu
kwa mahojiano kutokana na kuhusika na tukio la kuchoma nyumba ya
aliyokuwa akiishi Katibu wa UVCCM.
0 comments:
Post a Comment