Aliyekuwa
Mbunge wa Jimbo la Siha kwa tiketi ya CHADEMA, Godwin Ole Mollel ambaye
alihama chama hicho na kujiunga na CCM amefunguka na kusema alipotoka
Bungeni wakati Rais Magufuli anaingia ulikuwa ni uamuzi wa kitoto.
Mollel
amesema hayo juzi wakati wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi wa marudio
ambao unatarajiwa kufanyika Februari 17, 2018 ambapo Mollel sasa
anagombea ubunge wa jimbo la Siha kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM).
"Nilipofika
Bungeni nikaambiwa ukimuona Magufuli anaingia Bungeni wewe toka nje,
nikabisha kidogo nikaambiwa wewe ambaye ni mbishi kwanza tangulia mbele,
kwa sababu mimi nina nidhamu na naheshimu viongozi nikatangulia
kikamanda mbele nikatoka nje, nikiumia nikisema nimefanya jambo la
kitoto lakini ikafika mahali nikaambiwa hauruhusiwi kuongea na Mbunge wa
CCM, wala kumsalimia" alisema Mollel
Mbali
na hilo Mollel anasema baadaye aliambiwa ashone suti ili siku bajeti
ikiwa inajadiliwa watoke nje lakini yeye anadai aligoma na kuanzia hapo
alianza kuchukiwa ndani ya chama chake hicho alichokihama.
Pia
Mollel amedai kuwa anatambua Lowassa atakuja kupiga kampeni za CHADEMA
Siha na kusema anatambua kiongozi huyo amepangwa na hawezi kukataa kwa
kuwa anaogopa kufukuzwa kwenye chama kwa kuwa tayari yeye ni mzee lakini
amesema alishawaeleza ukweli kutoka Ikulu kwamba CCM ndiyo mpango.
0 comments:
Post a Comment