Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli leo Januari
23, 2018 ametengua uteuzi wa Mkurgenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Butiama, Solomoni Kamlule Ngiliule kutokana na kushindwa kutimiza
majukumu yake kama ilivyopaswa.
Waziri
wa nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za Mitaa
(TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza na waaandishi wa habari,ametangaza
uamuzi huo leo, zikiwa zimepita siku tatu tangu Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa alipotoa maagizo kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bw.
Raphael Nyanda kutuma timu ya wakaguzi kwenda kufanya ukaguzi maalumu
katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Butiama.
“Kutokana
na hali iliyojitokeza Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe
Magufuli ambaye pia ndiye Waziri mweye dhamana wa Ofisi ya TAMISEMI,
amechukua fursa hiyo baada ya yaliyojiri Mkoa wa Mara, hasa katika
Halmashauri ya Butiama, Amemtengua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Butihama, Ndugu Solomoni Kamnule Ngiriule, kuanzia leo hii kutokana na
kushindwa kutimiza majukumu yake kama mkurugenzi mwenye dhamana,”
amesema Waziri Jafo.
Waziri
Jafo amemtaka Katibu wa TAMISEMI kuchukua hatua dhidi ya mweka hazina
aliyekuwapo kipindi ambacho ubadhirifu huo ulipotokea.
“Na
hata hivyo namuelekeza Katibu Mkuu TAMISEMI kuchukua hatua stahiki kwa
mweka hazina wa Halmashauri ya Butihama ambaye alikuwepo kipindi hicho
ubadhirifu ulipokuwa unatokea,” amesema Waziri Jafo.
Kufuatia
hatua hiyo, Waziri Jafo amewataka watendaji wote wa Wizara yake
kuhakikisha kuwa wanatimiza majukumu yao ipasavyo, kwani walipewa jukumu
la kuwatumikia wananchi na siyo jambo jingine.
“Hata
hivyo niwatake watendaji wote wa TAMISEMI kuhakikiha kwamba wanatimiza
wajibu wao kwa dhamana kubwa waliyopewa kwa ajili ya kuwatumikia
watanzania,” amesema.
0 comments:
Post a Comment