Msimamizi
wa uchaguzi wa jimbo la Kinondoni ambaye pia mkurugenzi wa manispaa
hiyo, Aron Kagurumjuli ameyatupilia mbali mapingamizi matatu
yaliyowasilishwa na wagombea wa vyama vya Chadema, CCM na CUF.
Mapingamizi
hayo ni kwa mgombea wa CUF, Rajab Juma kumwekea mgombea wa Chadema,
Salumu Mwalimu, wakati Mwalimu yeye alimwekea Maulid Mtulia wa CCM na
mgombea huyo wa chama tawala alimwekea mgombea wa SAU, Johnson Mwangosi.
Baada
ya jana ofisi ya msimamizi wa uchaguzi kutoa barua ya utetezi kwa
wagombea waliowekewa mapingamizi leo Jumanne imetoa majibu ya
kuyatupilia mbali mapingamizi hayo.
“Tumeyatupilia
mbali mapingamizi yao kwa sababu hayana mashiko, kilichobaki ni
wagombea kwenda uwanjani wakapambane,” amesema msimamizi huyo.
0 comments:
Post a Comment