Jaji
Mkuu wa Tananzania, Profesa Ibrahimu Juma amewataka viongozi wa
serikali na vyama vya siasa kuacha mara moja vitendo vya kuingilia
mhimili wa Mahakama na kuvunja amri zake.
Jaji
Profesa Juma ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu wiki ya Sheria inayotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi
ujao (Februari mosi), siku ambayo ndio itakayoashiria kuanza rasmi kwa
shughuli za Mahakama kwa mwaka huu 2018 yatakayofanyika katika viwanja
vya Mahakama vilivyopo mtaa wa Chimala jijini Dar es Salaam, ambapo
mgeni rasmi atakuwa Rais John Magufuli.
"Kwa
mujibu wa Katiba ya Tanzania mamlaka ya utoaji haki ni ya Mahakama tu,
nawasihi viongozi wote wa serikali wenye mamlaka za kikatiba na kisheria
wabaki ndani ya maeneo yao ya Kikatiba na wajiepushe kuingilia maeneo
yaliyo ndani ya haki, hadhi na Mamlaka ya Kikatiba ya Mahakama", alisema
Jaji Profesa Juma.
Kwa
upande mwingine, Jaji Profesa Juma ametoa rai kwa wananchi na wadau
wote wa sheria kutembelea Mnazi Mmoja kwa ajili ya kujifunza na kupata
huduma mbalimbali za Kisheria kutoka kwa Majaji, Mahakimu, Wasajili,
Watendaji, Mawakili wa serikali na Mawakili wanaojitegemea ambao
watakuwa tayari kuwasikiliza na kuwahudumia ipasavyo.
0 comments:
Post a Comment