Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum Jijini Dar es salaam Lazaro Mambosasa, amesema
wahalifu waliotoka jela kwa msamaha wa Rais hawatasita kuwarudisha tena
jela iwapo wataendelea na tabia za uhalifu.
Kamanda
Mambosasa ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na waandihsi wa
habari alipokuwa akiwapa taarifa za uhalifu, na kusema kwamba watu
wanaoongoza kwa vitendo vya uhalifu ni wale waliotoka kwa msamaha wa
Rais, na kwamba wanatumwa na wenzao walio jela.
Akiendelea
kuzungumzia suala hilo Kamanda Mambosasa amesema watu hao wamekuwa
wakirudia maeneo walioficha silaha kabla hawajakamata na kufungwa, na
kuzichukua kuzitumia kwenye matukio ya uhalifu, huku wakendelea
kuwasiliana na wale ambao bado wako gerezani kujua wameweka wapi silaha
ili kuzitumia kwenye kazi zao, na kisha kuwapelekea posho.
“Taarifa
tulizonazo baada ya wahalifu wengine waliochiwa kwa msamaha wa Rais,
wachache hawataki kubadili tabia zao, wanakwenda kufichua silaha ambazo
walilizika ardhini na sasa wanazifukua kwa ajili ya kuanza kuzitumia.
Ninatoa onyo kwa mtu yeyote ambaye amepata msamaha, badala ya kumshukuru
Mungu akabadili tabia akaanza kuishi kwa kufuata sheria za nchi,
anaenda kufukua silaha mahali alipoficha kwa ajili ya kuendeleza vitendo
vya uhalifu, niwaambie hawatabaki salama, tutawarudisha huko
walikotoka”, amesema Mambosasa.
Kufuatia
tukio hilo Kamanda Mambosasa amewataka watu waliopewa msamaha na Rais
na kuwa huru, uacha kabisa matendo maovu, na kuwaomba wananchi kutoa
ushirikiano pale wanapohisi kuna mtu anafanya vitendo vya uhalifu.
0 comments:
Post a Comment