Mamia ya wanawake wanatarajia
kukutana Jijini Mbeya kwaajili ya kuadhimisha siku ya wanawake Duniani Tarehe
8/03/2018 ndani ya ukumbi wa Tugimbe saa nane kamili mchana (8:00 AM) ambapo
pamoja na kukutana pia watatoa misaada kwa watoto wanaoishi katika mazingira
magumu, pamoja na yatima jijini hapo.
Akizungumza na AFRICAN NEWS
BLOG,Bi,LIDIA MTELIKI ambaye ndiye mratibu wa Kusanyiko hilo,amesema kila mwaka
wanawake wa jiji la Mbeya hukutana kwa lengo la kuadhimisha siku ya mwanamke
Duniani katika kusanyiko hilo huwa na mambo kadhawakadha ikiwemo kuendesha semina
ya ndoa,kutoa misaada kwa wasio jiweza,watoto waishio katika mazingira magumu
pamoja na yatima.
Bi,Mteliki ameongeza
kuwa siku hiyo kutakuwa na Walimu walio
bobea katika kutoa Elimu ya maisha ya mwanamke katika ndoa pamoja na burudani,
pia wanawake watapewa fulsa ya kutoa mawazo yao katika kuelekea nchi ya viwanda
na uchumi wa kati katika kumwinua mwanamke.
Aidha Bi,Lidia Mteliki
ametowa wito kwa wanawake wote kushiriki kusanyiko hilo,huku akibainisha mikoa
na nchi zitakazo shiriki ikiwemo,mikoa ya Mbeya, Arusha,Iringa,Songea,Rukwa
pamoja na nchi za Malawi,Zambia nk.
0 comments:
Post a Comment