Jeshi
la Polisi Kigoma limemzuia Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kufanya
mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Uwanja wa Mwanga Community Center,
mkoani Kigoma ambao ulipaswa kufanyika leo Januari 16, 2018.
Taarifa
iliyotolewa na OCD inasema kuwa kiongozi huyo hakufuata utaratibu wa
kutoa taarifa ndani ya masaa 48 kabla ya kufanyika kwa mkutano huo jambo
ambalo Mbunge Zitto Kabwe amelilamikia na kusema kuwa amezuiwa kufanya
Mkutano kinyume na sheria ya Bunge ya mwaka 1988.
"Mimi
sitaki kuwapa polisi sifa ya kupambana nasi. Tumeahirisha mkutano mpaka
siku ya jumamosi Lakini tumewaandikia barua rasmi kuwa sheria
waliyonukuu sio sheria halali na haihusiani na mikutano ya Mbunge kwenye
jimbo lake la Uchaguzi. Sheria wanayopaswa kunukuu ni sheria namba 3 ya
mwaka 1988 kifungu cha 4(1)". Alisema Zitto Kabwe
Kufuatia
jambo hilo Zitto Kabwe amedai kuwa atamwandikia barua rasmi Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai kuhusu suala
hilo ili kutengeneza mazingira kwa siku za usoni lisije kumtokea Mbunge
mwingine yoyote.
Hata
hivyo kupitia ukurasa wake wa facebook ameambatanisha na nyaraka
inayompa mamlaka ya kuendesha mikutano ndani ya Jimbo lake.
0 comments:
Post a Comment