Nyumba
ya Katibu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wa Mkoa wa
Iringa, Alphonce Muyinga iliyopo maeneo ya Kihesa njiapanda ya Kwabeda
imechomwa moto na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.
Ambapo
kikosi cha Zima Moto kilifanikiwa kufika katika nyumba hiyo na kujaribu
kuzima moto huo ambao tayari ulikuwa umeshaleta athari ndani ya nyumba
hiyo kwa mali mbalimbali zilizokuwepo ndani.
Pia
aliyekuwa Diwani wa kata ya Mwangata, Iringa kwa tiketi ya Chadema na
baadaye kujiuzulu nafasi yake hiyo, Anjelus Mbogo naye amefanyiwa
uharibifu katika nyumba ambayo alikuwa akijenga baada ya watu
wasiojulikana kuibomoa nyumba hiyo.
Anjelus amedai kuwa tukio hilo linawezekana kuwa limetokea kutokana na matamko ya uchochezi yaliyotolewa na Mbunge kwa wananchi.
“Kauli
ya Mbunge ndiyo inaweza kuwa chanzo cha uchochezi kwa wananchi kuja
kubomoa nyumba hizi kwa sababu yeye aliwaambia wananchi kama atajiuzulu
wabomoe nyumba yake hata gari yake ichomwe moto nadhani wananchi
wakachukua hilo kwani wananchi unapowashawishi ndivyo unavyomuaminisha
kuja kufanya hivi huo ndiyo ukweli. Na mimi sisemi mambo mengi kwa kuwa
jambo hilo bado linaendelea na upelelezi lakini naamini wameniaminisha
kuwa hatabaki mtu” amesema Anjelus Mbogo
Aidha amesema hawezi kuongea mengi zaidi kwani swala hilo linafanyiwa upelelezi kubaini watu hao wasiojulikana.
0 comments:
Post a Comment