Wizara
ya Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa nchini Afrika Kusini imemwita
Naibu Balozi wa Marekani, jijini Pretoria kufuatia matamshi ya Rais
Donald Trump wa nchi hiyo kuhusu nchi za Afrika.
Rais Trump anaripotiwa kuyataja mataifa ya Afrika kuwa machafu wakati wa mahojiano yake kuhusu sera za uhamiaji.
Amewaambia waandishi wa habari kuwa yeye sio mbaguzi.
Taarifa
kutoka ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Afrika Kusini inasema kuwa
inaunga mkono taarifa iliyotolewa na Muungano wa Afrika.
Au ilielezea mshangao wake kutokana na matamshi hayo na kumtaka Trump kuomba msamaha.
Afrika Kusini inasema kuwa uhusiano wake na Marekani unastahili kuwa katika misingi ya heshima.
Namibia, Botswana na Ghana ni baadhi ya nchi ambazo zimetoa taarifa za kumshutumu vikali Rais Trump.
Credi: BBC
Credi: BBC
0 comments:
Post a Comment