Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kesho inakutana katika kikao cha ‘dharura’ jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar, Salum Mwalimu amesema lengo la kikao hicho ni kufanya tathmini ya hali ya kisiasa nchini.
Alipotakiwa
kueleza kama lengo la kikao hicho ni kujadili ziara ya waziri mkuu wa
zamani, Edward Lowassa kwenda Ikulu, Mwalimu amesema kikao hicho si cha
dharura kwani kilipangwa kufanyika Desemba mwaka jana lakini
kiliahirishwa kutokana na sikukuu za mwisho wa mwaka.
Amesema
ajenda za kikao hicho zilipangwa kabla Lowassa ambaye ni Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Chadema hajaenda Ikulu hivyo hakina uhusiano na ziara hiyo
ila huenda jambo hilo likajitokeza.
“Suala hilo halipo kwenye ajenda ila linaweza kujitokeza na likijitokeza litazungumziwa lisipojitokeza basi,” amesema Mwalimu na kuongeza;
“Hata hivyo kwa upande wake inaweza kuwa fursa nzuri kuielezea Kamati Kuu na viongozi wenzake nini kilitokea.”
0 comments:
Post a Comment