Mama
watoto wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady amempongeza muimbaji
huyo mara baada ya kuweka wazi ujio wa kituo chake cha redio na runinga.
Katika
pongezi hizo Zari amemtaja Diamond kama mtu anayejituma zaidi katika
kile anachokifanya. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zari ameandika;
Hongera
Damond Patnumz sana kwa juhudi na bidii uliyonayo Allaah akujalie kwa
mengine mazuri zaidi. Siku zote umekuwa mpiganaji wa kazi zako, kwa kuwa
njia pekee ya kuijenga familia ni kupiga KAZI najua malengo yako
Alhamdulillah! #wcbTV #wcbFILMSTUDIO #wcbMUSICSTUDIO #wcbRADIO
#wcbHEADQUATERS.
Bila kusahau #DiamondKaranga na chibuperfume #ChibuPerfume 2018 looking good👌🙏
Hapo
jana Diamond aliachia video mtandaoni ikionyesha mjengo mpya wa WCB
ambao utatumika kama makao makuu ya kampuni hiyo pamoja na studio za
Wasafi TV na Wasafi Redio.
Pia utakumbuka hii si biashara ya kwanza kwa Diamond kwani ameshaingiza sokoni manukato yake ‘Chibu Perfume’ pamoja na Karanga.
0 comments:
Post a Comment