Chama cha ACT Wazalendo kinawatakia Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla maadhimisho mema ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Taarifa
kutoka kwa Chama hicho imeeleza kuwa maadhimisho haya ya Mapinduzi ya
Zanzibar yawe kichocheo cha kuimarisha misingi ya undugu.
==>Soma taarifa kamili;
SALAMU ZA MAPINDUZI KUTOKA ACT WAZALENDO
Chama cha ACT Wazalendo kinawatakia Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla maadhimisho mema ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Maadhimisho
haya ya Mapinduzi ya Zanzibar yawe kichocheo cha kuimarisha misingi ya
undugu, umoja na mshikamano miongoni mwa Wazanzibari na Watanzania kwa
ujumla.
Kwa
Wazazibari, Miaka 54 ya Mapinduzi iwe fursa maridhawa ya kufanya
tafakari na tathmini ya kina. Ni kipindi cha kujiuliza maswali. Je
malengo ya Mapinduzi ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuleta haki na usawa
yamefikiwa? Vipi kuhusu ustawi wa Zanzibar? Ni kwa kiwango gani
Mapinduzi ya Zanzibar yameleta maendeleo yaliyokusudiwa ya kiuchumi na
kijamii kwa Wazanzibari Wote?
Ujumbe
wa Chama chetu kwa Wazanzibar ni kuwa ustawi wa Zanzibar unahitaji
jitihada za Wazanziabari Wote bila kujali tofauti za kisiasa.
Maadhimisho ya 54 ya Mapinduzi yawakumbushe Wazanzibari umuhimu wa
maridhiano ya kisiasa na kuimarisha undugu kwa ajili ya ustawi wa
Zanzibar.
Juma Said Sanani, Makamo Mwenyekiti, ACT Wazalendo, Zanzibar.
12 Januari 2018
0 comments:
Post a Comment