Bunge
bado halijamuandikia barua ya kumuita Mkuu wa Mkoa wa Njombe,
Christopher Ole Sendeka ili kujibu tuhuma za kukejeli na kudharau
muhimili huo.
Katibu wa Bunge Stephen Kigaigai amesema kuwa bado hawajamuandikia barua ya kumwita kufika katika kamati hiyo.
"Niko katika kikao lakini ninachofahamu kuwa bado hatujamuandikia," amesema Kigaigai.
Januari
9 mwaka huu Spika wa Bunge, Job Ndugai aliagiza Kamati ya Haki, Maadili
na Madaraka ya Bunge kumuita na kumhoji Sendeka wakati wa uchunguzi wa
kamati hiyo kuhusu tuhuma hizo zilizonukuliwa katika mitandao ya jamii
kwa lugha ya Kimasai, Kiswahili na Kingereza.
Spika
alisema lengo la kumuita ni kubaini ukweli wa dhamira ua kauli hizo na
lutoa mapendekezo kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa na Bunge.
0 comments:
Post a Comment