Mbunge
wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amepelekwa mahabusu katika Gereza la
Ruanda mkoani Mbeya baada ya kukosa dhamana katika kesi ya uchochezi
inayomkabili.
Sugu
na Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga
wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya leo Januari 16 na
kupelekwa mahabusu leo Jumanne Januari 16, baada ya Wakili wa Serikali,
Joseph Pande kuiomba mahakama kuzuia dhamana kutokana na usalama wa
washtakiwa kutokana na kosa walililotenda.
“Kosa
walilolitenda washtakiwa ni kutoa maneno ya fedheha yanayomtaja rais
kuwa muuaji hivyo wakiwa nje wanaweza kupata matatizo kwa wananchi ambao
hawajapendezwa na maneno hayo,” alidai Wakili Pande.
Hakimu
Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite alikubaliana na ombi hilo ambapo
aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 19, mwaka huu atakapotoa uamuzi wa
dhamana.
Washtakiwa
hao wanadaiwa kufanya uchochezi kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya
Rais John Magufuli, Desemba 30, mwaka jana akiwa katika viwanja vya
mikutano vya shule ya msingi Mwenge iliyopo jijini Mbeya ambapo Sugu
anadaiwa kutamka kuwa rais ni muuaji.
0 comments:
Post a Comment