Waziri
mkuu wa zamani Edward Lowassa amekutana na mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe ili kumpa mrejesho wa alichozungumza na Rais John
Magufuli.
Taarifa
iliyotolewa leo Alhamisi na Msemaji wa Lowassa imeeleza kuwa kumekuwa
na waraka na taarifa nyingi za kupotosha umma kuhusu ziara ya Lowassa
kwenda Ikulu na nyingine zikisemwa zimetoka kwa msemaji wake.
“Taarifa
zote hizo siyo kweli na wala siyo rasmi kutoka ofisini kwa Mh Lowassa.
Baada ya ziara ile, Mhe Lowassa alikutana na mwenyekiti wa chama chake,
Mhe Freeman Mbowe na kumpa mrejesho wa yaliyojiri Ikulu.”
“Kumekuwa
na taarifa nyingi kwenye mitandao zikiwemo kufunguliwa kwa akaunti
mbalimbali feki , taarifa zote hizo zipuuzwe kwani zina lengo la
kupotosha kwa malengo wanayoyajua wapotoshaji hao pamoja na mawakala
wao,”
“Taarifa rasmi zitatolewa kwa njia rasmi na watu wenye mamlaka hiyo.poleni kwa usumbufu wote.”
============================
0 comments:
Post a Comment