Mbunge
wa Geita, Joseph Msukuma amesema kwamba viongozi wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo wanapiga kelele kwenye mitandao ya kijamii
kuhusu Lowassa kwenda Ikulu lakini hawana mabavu ya kumfukuza uanachama
kwani yeye ndiye mwenye chama.
Msukuma
amedai kwamba, Mbowe ambaye anaaminiwa kuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA
tayari alikwishauza chama kwa Lowassa muda mrefu ndiyo maana hana sauti
ya kumuwajibisha.
Aidha
Msukuma hajaishia hapo ambapo pia amemtaka Mbowe ambaye ni Mwenyekiti
wa Chama hicho aoneshe nguvu yake ndani ya chama kwa kumwambia Lowassa
aombe radhi na siyo waombane wao kwa wao kwani kutakuwa ni kuwapumbaza
wanachama na wafusi wao bali hadharani watu waone.
"Lowassa
ndiye mwenye Chama. Wewe mbowe uliuza chama sasa wewe kama msemaji toa
kauli ya kumfukuza chama Lowassa. Tunashangaa kuanza kuchafuliwa kwa mtu
ambaye mlituaminisha kuwa anafaa kuwa Rais. Muite Lowassa umhoji
mitandaoni tuone akikuomba radhi. Na hata akikuomba radhi sasa hivi
tutajua siyo kwa mapenzi yake," Msukuma.
Ameongeza
kuwa, "Mbowe kusema kuwa Lowassa alikurupuka ni kumkosea adabu kwanza,
Lowassa ni mtu mzima kwake na yeye bado ni kijana. Na ninaamini kwamba
wewe Mbowe Lowassa hakuombi msamaha kwa kuwa yeye ndiye mmiliki".
0 comments:
Post a Comment